Habari kwa Umma
Tangazo kwa umma
ZOEZI LA UKAGUZI NA HESABU ZA KUFUNGA MWAKA 2025/2026 (STOCK TAKING)
Dar es Salaam, 11 Juni, 2026
Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) unapenda kuzijulisha taasisi za umma kuwa kutakuwa na zoezi la ukaguzi na hesabu za kufunga mwaka 2025/26 katika vituo na maghala yake yaliyoko katika mikoa yote Tanzania Bara.
Zoezi hili litaanza Jumatatu tarehe 22 Juni, 2026 mpaka Jumanne tarehe 30 Juni, 2026 kwa ofisi za mikoa ya Dar es salaam na Dodoma. Zoezi hili kwa mikoa mingine litaanza Alhamisi tarehe 25 Juni, 2026 mpaka Jumanne tarehe 30 Juni, 2026.
Aidha, tunatoa taarifa kuwa kwa siku ya Jumanne tarehe 30 Juni, 2026 huduma zote katika ofisi zote za GPSA mikoa zitatolewa kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni. Baada ya hapo, huduma zitasitishwa kwa muda kuanzia saa 12:00 jioni tarehe 30 Juni, 2026 mpaka saa 1:30 asubuhi tarehe 1 Julai, 2026 ili kukamilisha zoezi la ukaguzi na hesabu za kufunga mwaka 2025/26. Huduma zitaendelea kutolewa kama kawaida kuanzia saa 1:30 asubuhi Jumatano tarehe 1 Julai, 2026.
Tunazishauri taasisi za umma kupata huduma na vifaa mapema kabla ya muda huo, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. Tunaomba radhi kwa changamoto yoyote inayoweza kujitokeza.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa mteja kupitia namba +255735005005.
Imetolewa na
KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO
WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI (GPSA)

