User Registration

or Cancel
News

TARATIBU ZA UNUNUZI WA PAMOJA WA MAGARI YA SERIKALI


Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) imepewa jukumu la ununuzi wa pamoja wa magari ya Serikali kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 katika kifungu Na. 50 kinachoelekeza Taasisi za Umma kutumia mfumo wa ununuzi wa pamoja wa Vifaa na Huduma Mtambuka yakiwemo magari. Aidha kanuni Na. 131 (4) (a) ya Ununuzi wa Umma (GN446) pamoja na Waraka wa Hazina Na. 3 wa Mwaka 2014/15 zinaelekeza taasisi zote kuwasilisha mahitaji yao ya vifaa na huduma mtambuka (VHM) kwa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), mahitaji haya ni pamoja na ununuzi wa magari.

Kuona taratibu za ununuzi wa pamoja wa magari ya Serikali, bonyeza hapa.