User Registration

or Cancel
News

UTARATIBU WA KUPATA HUDUMA YA VIFAA KUTOKA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Wakala husambaza Vifaa na huduma kwa Wizara, Idara, Serikali za Mitaa na taasisi za umma kupitia ofisi zake zilizoko katika  Makao Makuu ya Mikoa yote ya Tanzania Bara.

Orodha ya vifaa hivyo ‘’stores catalogue’’ inapatikana katika tovuti ya Wakala www.gpsa.go.tz na  machapisho yanayotolewa na  Wakala.

Ili kupata vifaa GPSA, yafuatayo yatapaswa kuzingatiwa na Mteja;

  1. Kuleta barua ya uhitaji wa kupata vifaa/huduma zitolewazo na Wakala
  2. Kuleta barua ya utambulisho wa maofisa watatu(3) hadi wanne(4) ambao watakuwa na wajibu wa kutia sahihi katika nyaraka za kuagiza na kupokea vifaa (Combined Requisition and Issue Note-CRIN).
  3. Nyaraka hizo ni lazima ziwe zimesainiwa na maofisa wawili kati ya hao waliotambulishwa na hivyo barua lazima ionyeshe majina, vyeo na sahihi zao.
  4. Barua hiyo iambatanishwe na picha ya mtumishi atakaye wajibika kuchukua vifaa kutoka katika maghala ya Wakala.
  5. Unawajibika kununua vitabu vya ‘Combined Requisition and Issue Note (CRIN)’ kutoka katika ofisi zetu za Wakala kwa ajili ya kuombea na kisha kupokelea huduma zetu. (CRIN) kwa sasa  kinauzwa Sh.12,800.00.
  6. Utapewa ‘Bill’ ili uweze kulipia amana kwenye akaunti za Wakala na kuweza kuanza kupata vifaa mara tu baada ya malipo kufanyika.
  7. Huduma zote zinatolewa kwa kutumia CRIN.

 

Kuona maelezo zaidI ya utaratibu huu,bonyeza hapa.