User Registration

or Cancel
News

UTARATIBU WA KUPATA HUDUMA YA MAFUTA KUTOKA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Wakala hutekeleza jukumu la utoaji wa mafuta kupitia Kituo cha mafuta cha Wakala kilichopo Kurasini (Kurasini Fuel Depot) kwa upande wa Dar es Salaam na kupitia katika vituo vilivyopo katika makao makuu ya mikoa 22 ya Tanzania Bara na Wilaya Moja (1)  ya Ileje. Wakala unaendelea na taratibu za  kufikisha huduma ya mafuta  katika mikoa mipya ya Geita, Njombe na Simiyu huku huduma za vifaa vya ofisi zikiendelea kupatikana kama kawaida.

Kwa Upande wa  Huduma ya Mafuta  hutolewa siku saba za  wiki kuanzia saa moja na nusu  asubuhi  mpaka saa kumi na mbili jioni ikiwemo siku za  sikukuu za Kitaifa.

Ili kupata huduma ya mafuta yafuatayo yatazingatiwa;

  1. Kwa Mteja ambaye hajawahi kupata huduma ya Mafuta kutoka kwa Wakala, atalazimika kuwasilisha barua ya utambulisho wa watia sahihi kwa nyaraka za miamala walioidhinishwa (majina na sahihi zao)
  2. Mteja Kununua  kitabu chenye nyaraka za kutolea vifaa/mafuta kinachoitwa “Combined Requisition and Issue Note, (CRIN) kwa sasa  kinauzwa Sh.12,800.00.
  3. Kujaza  seti moja na nyaraka hiyo ikionyesha makadirio ya kiasi cha mafuta atakachowekea amana katika akaunti itakayofunguliwa katika mfumo wetu wa uuzaji wa mafuta.
  4. Taasisi inapolipia hupewa nyaraka ya uthibitisho wa mapokezi ya fedha  ambapo baada malipo hayo kufanyika, taarifa  huingizwa katika mfumo wa kuuzia mafuta.
  5. Baada ya kufanya malipo (amana) mteja ataendelea kutumia mafuta yake kwa kadri ya mahitaji yake kwa kuzingatia amana yake.
  6. Endapo Mteja atahitaji kupata mafuta katika kituo kingine cha Wakala tofauti na Kituo alicholipia mafuta, atalazimika kuwasilisha taarifa hiyo kwa kituo cha Wakala chenye akaunti yake kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na kituo (Mkoa) ambao mteja ataenda kupata mafuta.

 

Kupata maelezo zaidi ya utaratibu huu, bonyeza hapa.