emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari kwa Umma

TANGAZO LA KUSOGEZWA MBELE KWA MARUDIO YA MCHAKATO WA ZABUNI ZA MIKATABA MAALUM NA KUSUDIO LA KUTOA TUZO (INTENTION TO AWARD) ZA MIKATABA MAALUM

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) anapenda kuwajulisha umma na wazabuni wote kuwa marudio ya mchakato wa zabuni kwa wazabuni waliokwama kutokana na changamoto za mfumo wa ‘TANePS’ pamoja na wale ambao hawakushiriki uliotarajiwa kutangazwa siku ya Jumatatu tarehe 10 Mei, 2021, umesogezwa mbele mpaka siku ya Jumatatu tarehe 17 Mei, 2021 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Tangazo kwa ajili ya kuanza marudio ya mchakato huu litatolewa siku ya Jumatatu 17 Mei, 2021 kwa zabuni zote na tarehe zake za mwisho za kuwasilisha kwa kila zabuni kwa ajili ya wale watakaokuwa wamekosa katika mchakato wa mwanzo pamoja na wale ambao hawakushiriki.
Pia Afisa Mtendaji Mkuu anapenda kuwajulisha umma na wazabuni wote kuhusu kusudio la kutoa Tuzo (Intention to award) kwa wazabuni walioshinda zabuni za Vifaa na Huduma Mtambuka (VHM) kupitia Mikataba Maalum kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zilizotangazwa mnamo mwezi Machi, 2021.
Orodha ya wazabuni walioshinda na walioshindwa na sababu za kushindwa kwao itapatikana kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 10 Mei, 2021 kupitia mfumo wa TANePS unaopatikana kwa anuani ya ‘www.taneps.go.tz’.
Kwa wale walioshindwa na wana nia ya kuomba tena, pamoja na waombaji wapya ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mchakato wa mwanzo wanaombwa kushiriki katika marudio kupitia tangazo litakalotolewa siku ya Jumatatu tarehe 17 Mei, 2021.