emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    UZINDUZI WA SERA YA TAIFA YA USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI YA MWAKA 2025

  • 20-Mar-2026

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ina furaha kutangaza uzinduzi rasmi wa Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya Mwaka 2025.

Sera hii mpya ni hatua muhimu katika kuimarisha mifumo ya ununuzi, usambazaji, na usimamizi wa rasilimali za umma ili kuhakikisha ufanisi, uwazi, na thamani ya fedha katika sekta zote za kiuchumi.

Maelezo ya Tukio:

  • Tarehe: Jumatano, Aprili 8, 2026
  • Muda: Kuanzia saa 2:00 Asubuhi
  • Mahali: Ukumbi wa Jakaya Covention Centre, Dodoma
  • Mgeni Rasmi: Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • ________________________________________

    Imetolewa na:

    Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

    Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA)