Huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo
Huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo ni moja ya majukumu ambayo GPSA inatakiwa kutoa kwa Taasisi za Serikali kwa mujibu wa Kanuni ya 124 (6) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, Tangazo la Serikali Na. 518 la 2024. Huduma zote za GPSA, ikiwemo ya Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo, zinatolewa kwa njia ya kielektroniki kupitia Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Taarifa wa GPSA (GIMIS), unaopatikana kupitia anwani "https://gimis.gpsa.go.tz/login". Mfumo huu ni wa kielektroniki na unaweza kufikiwa kupitia kifaa chochote cha kielektroniki, na kupata huduma katika kituo chochote cha GPSA katika Mikoa yote.