emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari kwa Umma

KUREJEA KWA MFUMO WA GIMIS

Tunapenda kuujulisha umma na wadau wetu wote kwamba huduma zote zitolewazo na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kupitia mfumo wa GIMIS zimerejea rasmi kuanzia leo Jumapili tarehe 2 Agosti, 2026 saa 4:01 usiku baada ya kukamilika kwa maboresho ya mfumo wa GIMIS ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma zake.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao umejitokeza katika kipindi hicho.

Tunawashukuru kwa uvumilivu, uelewa na ushirikiano wenu.

Asante kwa kutumia huduma za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Imetolewa na;

KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO

WAKALA WA HUDUMA ZA UNUNUZI SERIKALINI