Habari kwa Umma
Tangazo kwa umma
MABORESHO YA MFUMO WA GIMIS
Dar es Salaam, Tarehe 30 Julai, 2026
Tunapenda kuwataarifu kwamba tutakuwa na zoezi la kuboresha mfumo wa GIMIS kuanzia tarehe 31 Julai, 2026, kuanzia saa kumi na mbili (12:00) kamili jioni hadi tarehe 02 Agosti, 2026 saa nne (4:00) kamili usiku.
Katika muda huo, huduma zote zitolewazo na Wakala kupitia mfumo wa GIMIS hazitopatikana. Maboresho haya ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi wa mfumo wa GIMIS na utoaji wa huduma za Wakala kupitia mfumo huu. Aidha, katika kipindi hicho wateja wote wa Wakala mnaombwa kuwasilisha mahitaji yenu ya huduma kupitia Meneja wa Mkoa husika kwa utaratibu mtakaoelekezwa.
Wakala unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki.
Kwa msaada zaidi tafadhali unaweza kuwasiliana nasi kwa kututumia barua pepe ya support@gpsa.go.tz au wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha mawasiliano kwa simu namba +255 735 005 005 kwa maelezo zaidi.
Asante kwa kutumia huduma za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Imetolewa na;
KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO
WAKALA WA HUDUMA ZA UNUNUZI SERIKALINI

