emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    UFUNGUZI WA KIKAO KAZI CHA KAMATI YA MAPITIO YA UANZISHWAJI WA SHERIA YA GPSA

  • 10-Jun-2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Bi. Dorothy Mwanyika amefungua rasmi Kikao kazi cha Kamati ya Mapitio ya Uanzishwaji wa Sheria ya GPSA kilichoanza siku ya Jumatatu tarehe 27/05/2024 katika ukumbi wa NSSF Mkoa wa Morogoro ambapo kikao kazi hiki kitafanyika katika kipindi cha wiki mbili.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Kamishna Ndugu Alex Haraba aliyemuwakilisha Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha. Aidha hafla hiyo imehudhuriwa pia na Viongozi Wakuu wa GPSA Makao Makuu.

Bi. Dorothy alibainisha kuwa GPSA imeendelea kukua kiutendaji kazi na mapato hivyo ni muhimu kufanya mapitio hayo ili kuhakikisha GPSA inakuwa endelevu.

Bi. Dorothy amepongeza juhudi na mabadiliko makubwa mpaka sasa ya GPSA,hivyo ni muhimu GPSA kuboreka kulingana na mabadiliko ya utandawazi na ushindani ili kuongeza ufanisi.

Bi. Dorothy alisema kuwa ana imani kubwa na Kamati kuwa itatekeleza wajibu wake na kushauri vizuri kutokana na uzoefu na ueledi wa wajumbe.

Aidha Bi. Dorothy alikumbusha watumishi kufanya kazi kwa ueledi,kushirikiana,uaminifu na ubunifu ili kuzidi kuisogeza mbele GPSA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mapitio ya Uanzishwaji wa Sheria ya GPSA Bw. Mathias Bazi Kabunduguru alimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Bi. Dorothy Mwanyika na kuahidi kutekeleza jukumu hili kwa uaminifu mkubwa ili kuleta tija kwa Wakala na Serikali kwa ujumla.

Aidha Bw. Matias alielezea historia na umuhimu wa shughuli za Taasisi kama GPSA ulimwenguni kote ikiwemo usalama wa Serikali.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA Prof. Geraldine Arbogast Rasheli alimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara pamoja na Kamati kwa kuitikia wito huu, na kubainisha kuwa awali Wakala ulikuwa ukijulikana kama "Bohari Kuu ya Serikali" mpaka ilipobadilishwa rasmi na kuwa GPSA tarehe 16 Juni,2008 ambapo ilirithi na kuongezewa baadhi ya majukumu.

Prof. Geraldine aliongeza kuwa GPSA ni Taasisi ya kimkakati katika kufanikisha shughuli za Kiserikali.