emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    KIKAO CHA BODI YA USHAURI YA WIZARA PAMOJA NA KUTEMBELEA KITUO CHA MTUMBA-DODOMA

  • 10-Jun-2024

Bodi ya Ushauri ya Wizara ilifanya kikao chake siku ya Jumatano tarehe 05/06/2024 katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Mkemia Mkuu wa Serikali na kisha kufanya ziara katika kituo cha Mtumba jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi Bi. Dorothy Mwanyika aliwapongeza wajumbe wa Bodi kwa kuteuliwa ambapo watahudumu katika kipindi cha miaka mitatu. Pia aliwapongeza Menejimenti ya Wakala kwa kazi nzuri ya kuboresha utoaji huduma pamoja na watumishi.

Aidha Bi. Dorothy alipongeza ujenzi wa vituo vidogo kama vile Mtumba kwenye maeneo ya kimkakati ili kurahisisha utoaji huduma na kuongeza mapato.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Prof. Geraldine Rasheli alimshukuru Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya Ushauri kwa maelekezo wanayotoa ili kuisogeza mbele Wakala.

Prof. Geraldine aliongeza kuwa pamoja na kuongeza mtandao wa vituo vya mafuta, Wakala umeanza kutoa huduma masaa 24 katika kituo cha Kisasa na lengo ni kufikia vituo vyote vya Wakala ikiwemo kuanza matumizi ya kadi itakayowezesha wateja kujihudumia hata baada ya saa za kazi.