emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari


GPSA imeungana na Wafanyakazi wote duniani katika maadhimisho ya siku ya Mei Mosi ambayo Kitaifa imefanyika jijini Arusha ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

GPSA ilishiriki maadhimisho haya kupitia Ofisi za Wakala katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Maadhimisho ya Mei Mosi huambatana na kutambua mchango wa wafanyakazi katika jamii, kusherehekea haki za wafanyakazi, mafanikio yao, na kusisitiza umuhimu wa haki na wajibu katika kazi.

Kauli mbiu ya Kitaifa ya maadhimisho haya 2024 ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga dhidi ya Hali ngumu ya Maisha“