emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari


Menejimenti ya GPSA na TANESCO zilikutana siku ya Ijumaa tarehe 15/09/2023 katika ukumbi wa mikutano wa GPSA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Kikao hiki kilihusu maboresho ya huduma ya mafuta inayotolewa na GPSA katika vituo vya TANESCO vya kuzalisha umeme katika Mikoa ya Kigoma, Mwanza na Katavi.

Katika kikao hiki Meneja wa Ofisi za GPSA Mikoa ya Kigoma, Mwanza na Katavi walishiriki pia.

Kikao hiki kiliongozwa na Bw. Mwakiselu Mwambange ambaye alieleza namna GPSA inavyowekeza kuboresha utoaji huduma zake na kuendelea kuwafikia wateja wengi zaidi ikiwemo miradi mbalimbali ya Serikali. Alieleza baadhi ya faida za kutumia huduma za GPSA ikiwemo gharama nafuu, usalama na uhakika.

Kwa upande wa TANESCO walishukuru na kumpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA Prof. Geraldine A. Rasheli pamoja na menejimenti nzima kwa huduma ya viwango vya juu wanayopata, ikiwemo kusikiliza wateja ambapo fursa hii ya kukutana na menejimenti ili kurekebisha changamoto ndogo ndogo itaongeza tija na kuisaidia Serikali na TANESCO kuhakikisha inayaangaza maisha ya Wananchi kwa uhakika.