emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    KUHITIMISHA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI (RISK MANAGEMENT TRAINING) KWA VIONGOZI NA WATUMISHI(RISK PIONEERS)

  • 23-Sep-2023

KUHITIMISHA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI (RISK MANAGEMENT TRAINING) KWA VIONGOZI NA WATUMISHI(RISK PIONEERS)

Mafunzo ya awamu ya kwanza ya usimamizi wa vihatarishi (Risk Management Training) ya GPSA ya siku mbili yamehitimishwa leo Jumamosi 09/09/2023 yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi mpya wa Mikutano wa ofisi ya GPSA Mkoa wa Pwani.

Akihitimisha mafunzo hayo ya awamu ya kwanza Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Bw. Moses Dulle alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA Prof. Geraldine A. Rasheli na menejimenti kwa kuwezesha mafunzo haya muhimu kwa Taasisi na kuwaasa kila mshiriki kutekeleza kwa vitendo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji ya GPSA Bw. Mwakiselu Mwambange kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu Prof. Geraldine Rasheli aliwashukuru wawezeshaji kutoka Wizara ya Fedha kwa mafunzo haya muhimu ambapo GPSA imekuwa miongoni mwa Taasisi za mwanzo kupata mafunzo haya, ambayo yatasaidia kuboresha uandaaji wa Mipango ya Wakala na utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi.