emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    MAFUNZO YA UELEWA WA ITHIBATI YA UBORA WA VIWANGO VYA KIMATAIFA (ISO)

  • 03-May-2024

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) imeendesha mafunzo ya uelewa wa Ithibati ya Ubora wa Viwango vya Kimataifa (ISO) leo Alhamisi tarehe 2 Mei,2024 katika ukumbi wa Chuo cha SUA (NCMC) katika Mkoa wa Morogoro.

Mafunzo haya ya siku moja yalifunguliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Prof. Geraldine A. Rasheli.

Akifungua mafunzo hayo, Prof. Rasheli amesisitiza umuhimu wa mafunzo haya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wakala 2023/24-2027/28 kuboresha huduma zake na kisha kupata cheti cha Uthibitisho wa Viwango vya Ubora wa Kimataifa (ISO).

Aliongeza kuwa cheti hiki kinaongeza uaminifu kati ya watumiaji,wateja na washirika wengine wa biashara/huduma na kuwezesha Wakala kutanua huduma zake na kufikia soko la Kimataifa.

Aidha Prof. Rasheli amewaasa viongozi na watumishi kuzingatia mafunzo haya ili kuongeza maarifa na ustadi muhimu ili kuongeza ufanisi na ubora wa utoaji wa huduma za Wakala.

Mafunzo haya yanatolewa na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS).