emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari


Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ulifanya mafunzo ya uelewa wa taratibu za Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo kwa meneja wa Mikoa yote yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha SUA(NCMC) katika Mkoa wa Morogoro.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Prof. Geraldine A. Rasheli alieleza maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika Wakala yaliyosaidia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo na kuwapongeza watumishi kwa bidii na ueledi katika utendaji kazi.

Prof. Rasheli alieleza kuwa huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji mizigo unaratibiwa katika Mikoa yote na kuwezesha wateja kupata huduma kwa wakati.

Prof. Rasheli alieleza kuwa Wakala katika Mpango Mkakati wake 2023/24-2027/28 katika sehemu ya Ugomboaji na Uondoshaji itaanzisha bandari kavu (ICD).

Prof. Rasheli aliwashukuru wadau walioshiriki kutoa mafunzo hayo ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).