emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    MAFUNZO YA VIASHIRIA VYA UDANGANYIFU (FRAUD RISK MANAGEMENT) KWA VIONGOZI WA GPSA MAKAO MAKUU NA MIKOA YOTE

  • 28-Nov-2023

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) umefanyamafunzo ya Viashiria vya Udanganyifu (Fraud Risk Management) kwa viongozi wa GPSA Makao Makuu na Mikoa yote yaliyofunguliwa na Bw. Abraham Msechu (Naibu Mkaguzi wa Ndani Mkuu) kutoka Wizara ya Fedha siku ya Ijumaa tarehe 24/11/2023 yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya GPSA Kibaha Pwani.

Bw. Msechu aliipongeza Wakala kwa kuwa miongoni mwa Taasisi za mwanzo kushiriki mafunzo haya, ambayo ni muhimu ili kuwezesha Taasisi kugundua viashiria na kuzuia ubadhirifu na hivyo kupunguza madhara kwa Taasisi husika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Prof. Geraldine A. Rasheli amewashukuru wawezeshaji kutoka Wizara ya Fedha kwa mafunzo haya, na kuahidi kuwa Wakala utatekeleza kwa vitendo mafunzo iliyopata na kuwa Taasisi ya mfano katika Viashiria vya Udanganyifu (Fraud Risk Management).

Mafunzo haya yanafanyika kwa siku mbili ambayo ni siku ya Ijumaa 24/11/2023 na Jumamosi 25/11/2023 katika Mkoa wa Pwani.