emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    MAKABIDHIANO YA MRADI WA UKARABATI KITUO CHA GPSA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

  • 10-Jun-2024

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumanne tarehe 21/05/2024 kati ya Meneja Ofisi ya Wakala Mkoa Dar es Salaam Bw. Joseph Matara na Mkandarasi Osaka Store yakishuhudiwa na TBA katika kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.

Bw. Matara akipokea mradi huu ambao umezingatia vigezo vya EWURA amemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Prof. Geraldine Rasheli kwa kusimamia maboresho ya utoaji wa huduma za Wakala kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Wakala wa miaka mitano (2023/24-2027/28).