emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari

    WAKALA WATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI JIJINI DODOMA

  • 06-Mar-2023

Watumishi wa ofisi ya Wakala wa Mkoa Dodoma walitembelea kijiji cha Matumaini St. Gasper Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 10/02/2023 kwa ajili ya kuwafariji na kuwasalimu watoto yatima wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Meneja wa ofisi ya Wakala mkoa wa Dodoma Bw. Presley Muro kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu alikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji ya kila siku ya watoto, chakula pamoja na kulipia Bima ya Afya kwa watoto 20.

Utoaji wa huduma kwa jamii (Corporate Social Responsibility) ni utekelezaji wa Lengo F la Mpango Mkakati wa Wakala.