emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI

Ununuzi Unaozingatia Thamani

Habari kwa Umma

KUANZA KWA MATUMIZI YA MFUMO JUMUISHI WA HUDUMA ZITOLEWAZO NA WAKALA – (GIMIS - GPSA INTEGRATED MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM)

1. Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) unapenda kuwatangazia taasisi zote za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinazopata huduma zitolewazo na Wakala, kuwa kuanzia tarehe 01/12/2021 ununuzi wa huduma za Wakala utafanyika kupitia mfumo jumuishi wa GPSA Integrated Management Information System (GIMIS), hii ni kufuatia kukamilika kwa mfumo huu uliojengwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

2.Mfumo huu unapatikana kupitia anuani ya https://gimis.gpsa.go.tz/login, na huduma zitakazotolewa kupitia mfumo huu ni pamoja na;-

i.Ununuzi wa Magari ya Serikali – Kuanzia maombi ya kibali, vigezo vya ubora (specifications), maombi ya usajili na usaijli wa gari husika;

ii.Ununuzi wa huduma ya mafuta (dizeli/petroli) kwa vyombo vya moto (magari, mitambo na pikipiki) pamoja na vifaa vya ofisi (shajala); na

iii.Ununuzi wa huduma ya Ugomboaji na Uondoshwaji (Clearing and Forwarding) wa mizigo kwa taasisi na watumishi wa umma pamoja na miradi inayotekelezwa na Serikali.

3.Mfumo huu utaanza kwa taasisi tisini (90) za awali ikifuatiwa na utaratibu endelevu wa usajili na utoaji wa mafunzo kwa taasisi zote zilizobaki zinazopata huduma katika Wakala kupitia ofisi za mikoa za Wakala kuanzia 01/01/2022. Ili kuweza kuona orodha ya majina ya taasisi zitakazoshiriki katika mpango wa mwanzo wa matumizi ya mfumo huu tafadhali gonga hapa. Aidha, kwa taasisi zilizochaguliwa kushiriki katika awamu hii ya mwanzo wanapaswa kujaza fomu ya usajili inayapatikana kwa ku gonga hapa.

Imetolewa tarehe 01/11/2021 na;

Prof: Geraldine A. Rasheli

AFISA MTENDAJI MKUU

WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKLIANI