Habari kwa Umma
Tangazo kwa umma
Mnamo siku ya Jumanne tarehe 18 Februari, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.
Paul Chacha akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora
alifanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini
(GPSA) Mkoa wa Tabora alitangaza kuwa amemuelekeza Katibu Tawala Mkoa wa
Tabora kumsimamisha kazi Meneja wa GPSA Mkoa wa Tabora Bw. Mayala Mburi
kupisha Uchunguzi wa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) unalaani na kukemea vitendo vya
aina yoyote vya utovu wa nidhamu katika Utumishi ambavyo ni kinyume na Sheria,
Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Wakala unaendelea na uchunguzi na
hatimaye kuzishughulikia tuhuma hizo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za
Utumishi wa Umma. Wakala umemsimamisha kazi Bw. Mayala Mburi ili kupisha
uchunguzi wa suala hilo na kumteua mara moja Bw. Stephen Muro kukaimu majukumu
ya nafasi hiyo na huduma zinaendelea.
Wakala unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Wakala utaendelea
kuhakikisha unazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma kwa
watumishi wake katika utoaji wa huduma zake na utachukua hatua stahiki kwa wale
wote watakaobainika kukiuka.
Wakala unawajulisha wateja wetu na Umma kwa ujumla kuendelea kuwasiliana nasi
kupitia mawasiliano yetu ya Kituo cha Huduma kwa Mteja namba 0735 005 005.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI