Ununuzi wa Pamoja wa Magari ya Serikali
Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 katika kifungu Na. 50 kinaelekeza Taasisi za Umma kutumia mfumo wa ununuzi wa pamoja wa Vifaa na Huduma Mtambuka yakiwemo magari. Aidha kanuni Na. 131 (4) (a) ya Ununuzi wa Umma (GN446) pamoja na waraka wa hazina na. 3 wa mwaka 2014/15 zinaelekeza taasisi zote kuwasilisha kwa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) mahitaji yao ya vifaa na Huduma Mtambuka ili kufanyiwa Ununuzi wa Pamoja.
Mchakato huu wa Ununuzi wa Magari ya Serikali unafanyika kidijitali kupitia mfumo wa kielektroniki wa “GPSA Integrated Management Information System-GIMIS” kwa anuani ya ‘https://gimis.gpsa.go.tz/login’.